𝐍𝐄𝐌𝐂 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐍𝐂𝐇𝐈𝐍𝐈 𝐊𝐎𝐓𝐄 𝐊𝐔𝐀𝐃𝐇𝐈𝐌𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐇𝐔𝐉𝐀𝐀


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeungana na Watanzania nchini kote kuadhimisha siku ya Mashujaa Tanzania katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Maadhimisho hayo kimkoa Dar es Salaam yamefanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila alioambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, Viongozi wa Vyama na Serikali, wakuu mbalimbali wa Taasisi.

Mhe. Albert Chalamila alifurahishwa na uwepo wa watumishi wengi wa Baraza katika maadhimisho hayo ikiwa ni taasisi pekee iliyoshiriki kwa wingi wa watumishi ambapo watumishi zaidi ya hamsini walishiriki.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa Tanzania hufanyika tarehe 25 Julai kila mwaka kuwakumbuka mashujaa waliopigania, kutetea na kuulinda uhuru wa Nchi yetu.